Msimu wa kuvuma kwa biashara zimerejea tena katika Bonde la Silicon. Bustani ya ofisi kando na Barabara kuu ya 101 kwa mara nyingine yamepambwa tena na hisia za biashara kuanza kushika kazi. Kodi imeanza kuongezeka, kama vile mahitaji ya nyumba za likizo za kifahari katika miji ya mapumziko kama Ziwa Tahoe, ishara ya utajiri unaokua. Eneo la Bay lilikuwa mahali tasnia ya umeme na kampuni za kompyuta na mtandao ambazo zimekua kutokana na hali hiyo. Wataalamu wake walianzisha teknolojia nyingi ambazo zinafanya ulimwengu kuwa ya kisasa, kuanzia kwa simu za kugusa-skrini hadi kutafuta mara moja maktaba kubwa hadi uwezo wa kuendesha ndege bila rubani kwa umbali wa maelfu ya maili. Kufufuliwa kwa shughuli zake za kibiashara tangu mwaka 2010 unaonyesha maendeleo imeshika kazi.
Kwa hivyo, inaweza ikashangaza kwamba watu wengine wanaoishi katika Bonde la Silicon wanafikiria mahali hapo imedorora, na kwamba kiwango cha uvumbuzi kimezembea kwa miongo kadhaa. Peter Thiel, mwanzilishi wa PayPal, na mwekezaji wa kwanza wa Facebook, anasema kwamba uvumbuzi huko Amerika unaendelea kufifia. Wahandisi katika kila kitengo wana hisia kama hizo za kufa moyo. Na kikundi kidogo lakini kinachokua cha wataalmu wa uchumi wanafikiria athari za kiuchumi za uvumbuzi wa siku hizi ni hafifu ikilinganishwa na yale ya zamani.
[…]
Kila mahali, uvumbuzi unaoendeshwa na nguvu ya usindikaji wa bei nafuu umeanza kushika kazi. Kompyuta zinaanza kuelewa lugha asilia. Watu wanadhibiti michezo ya video kupitia kwa mwendo wa mwili pekee - teknolojia ambayo inaweza kupata matumizi katika sehemu nyingi za ulimwengu wa biashara. Uchapishaji wa kivimbe- tatu unaweza ukatoa vitu kadhaa changamani, na hivi karibuni huenda ukahamia kwa misuli ya kibinadamu na vitu vingine vya kikaboni.
Msorajua wa uvumbuzi anaweza kupuzilia mbali hayo kuwa ni ya uwongo. Lakini wazo kwamba ukuaji unaoongozwa na teknolojia lazima uendelee bila kutatizwa au kupungua kwa utaratibu, badala ya kufifia na kurejea kwa kishindo, haupatani na historia. Chad Syverson wa Chuo Kikuu cha Chicago anasema kwamba ukuaji wa tija wakati wa ujanaji ulikuwa na matatizo mengi. Ukuaji ulikuwa polepole wakati wa uvumbuzi muhimu wa bidhaa zinazotumia umeme mwishoni mwa karne ya 19 na mapema karne ya 20; na kisha kukua kwa haraka.